Tunashuti sherehe mbali mbali na tuna shuti video aina zoote Ze Make Official Entertainment

6 Apr 2014

20% ANASWA KWA MGANGA WA KIENYEJI, YADAIWA ALIPELEKWA NA PAPAA MISIFA. SOMA HAPA

Makubwa! Kichwa cha Bongo Fleva kutoka pande za Kimanzichana mkoani Pwani, Abas Kinzasa ‘20%’, anadaiwa kunaswa laivu akiwa kwa mganga wa kienyeji akipata tiba ya kupunguza na kuondoa sumu ya utumiaji wa bangi na pombe, Ijumaa Wikienda lina ‘pakeji’ kamili.
Abas Kinzasa ‘20%’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, ishu hiyo ilijiri katika Kijiji cha Ngukumo mkoani Tabora baada ya mameneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Papa Misifa na Steve Mbaga kumshika mkono 20% na kutafuta mganga wa kienyeji ambaye aliwatangazia kuwa ana dawa zinazoweza kumuondoa sumu hiyo.
Baada ya kunyetishiwa stori hiyo, gazeti hili liliwatafuta mameneja hao ambao walisema walilazimika kufanya hivyo ili waweze kumrudisha 20% kwenye gemu kwa mara nyingine kwani bado wanaamini ana uwezo mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.
“Kiukweli mimi na mwenzangu tumekuwa tukisikitishwa kwa muda mrefu baada ya 20% kubobea kwenye matumizi ya pombe na bangi na hasa alipozidiwa hadi akashindwa kufanya muziki huu ambao tunaamini kwake ndiyo ilikuwa ajira pekee.
“Kwa kutambua hilo tulimtafuta na kuongea naye, alipokubaliana nasi tukaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji, ameshapata tiba na tayari ameonyesha kujitambua, hivyo hivi karibuni tunaanza kufanya naye kazi na ndiyo tunatoka kumlipia nyumba ya kuishi maeneo ya Mwananyamala Hospitali,” alisema Papa Misifa.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta 20% ambaye mwaka 2011 alichukua tuzo tano za Kili na kumuuliza juu ya suala hilo ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Papa Misifa na Steve Mbaga wamejitahidi sana kunifanya niachane kabisa na matumizi ya pombe maana walinipeleka kwa mganga wao ambaye kweli amenisaidia.
“Ujue kilichokuwa kikiniyumbisha siku zote hizo ilikuwa ni pombe maana bangi ilikuwa si kiivyo, nilipokuwa nakunywa pombe kweli ilikuwa ikinitoa kwenye njia na kunifanya kujiona mimi ndiyo mimi kiasi cha kushindwa hata kuwaheshimu wenzangu na ndiyo jambo pekee ninaloweza kusema limenifanya kuwa hivi.”

No comments:

Post a Comment

 

Luka Lee ft Young Rafa

Live Score

oka d ft jos p