Miaka mitatu nyuma wakazi na wapenda burudani wa Mwanza na kanda ya ziwa walimfahamu baada ya kuachia ngoma ya “So fine” akiwa chini ya usimamizi wa studio za Rock town records kwa mkataba usio rasmi, anaitwa Baraka da Prince. Wiki hii CEO wa studio za Tetemesha Records Sandu George a.k.a Kidboy ameamua kuweka wazi uhusiano wa msanii Baraka da Prince na Studio za Tetemesha Records.
Amekua chini ya Tetemesha toka mwaka jana lakini kwa kawaida kabla ya kumtoa hadharani msanii mpya hua kuna utaratibu wa ndani katika hatua za kumuandaa ndio sababu ninamtambulisha sasa.
Tegemeeni Video na Audio muda si mrefu kutoka sasa, Video imefanywa na Nisher. Itatangulia kutoka video kisha baada ya wiki itafuata Audio.
Mawasilano ya Barakah:
Simu: 0714 321086
Insta: @barakah_daprince
Twitter: @barakahdaprince
FB: Barakah da Prince
Best Regards
Kidboy
No comments:
Post a Comment