Baada ya ukimya wa muda mrefu rapper toka Tongwe Records, Roma Mkatoliki ataachia wimbo wake mpya wiki ijayo alioupa jina la ‘KKK’ ikiwa ni sehemu ya mradi wake wa mwaka huu alioupa jina la ‘The Return of The Ninja.’
Roma ameweka wazi mpango wake kupitia kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times kinachoongozwa na Jabir Saleh aka Kuvichaka.
“Tunaplan kuitoa siku yoyote kuanzia wiki ijayo yaani kuanzia jumatatu. Inaweza kuwa Jumatatu hiyo hiyo ama jumanne, ama jumatano. Kwa nini hatuko sure…kwa sababu Tongwe kuna wasanii wengi ambao wanatakiwa kutoka pia...ndo maana hatuko sure na tarehe lakini tuko sure na wiki. Wimbo utatoka wiki ijayo, unaitwa ‘KKK’ yaani triple K, umefanyika Tongwe records kwa producer J-Ryder pamoja usimamizi mzima wa C.E.O wetu wa Tongwe ambaye ni J-Marder.” Amesema Roma.
Rapper huyo wa ‘2030’ aliongelea pia ujio wa mradi wake mpya alioupa jina la ‘The Return of The Ninja’ kwa mwaka huu na kudai kuwa amebadilisha mfumo aliokuwa nao wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka, na sasa atakuwa anatoa nyimbo tatu kwa mwaka.
“Kilichofanyika ni kwamba 2030 ndo ni kama nilikuwa nimefunga hivi kitu ambacho nilikuwa nimekianza, nikiwa ninamaanisha kwamba kama ni album ambayo ilikuwa inatakiwa kutoka basi ilifungwa kwa kutoa 2030 ambayo niliitoa mwaka 2012 mwishoni kuelekea 2013.” Roma aliiambia The Jump Off.
“Kwa takribani miaka sita ama saba nilikuwa na system hiyo ya kutoa wimbo mmoja kwa mwaka toka 2007 tunaanza na wimbo wa kwanza. Lakini time inaenda na vitu vingi vinaenda vinabadilika. Kwa hiyo kitu ambacho Roma anakuja nacho 2014 hatatoa wimbo mmoja kama ilivyozoeleka, nina plan ya kutoa nyimbo kama tatu kwa sababu nyimbo zinarekodiwa kila siku. Kwa hiyo wimbo wa kwanza tunautoa mwanzo wa mwaka, katikati ya mwaka kwenye June hivi naweza kutoa wimbo mwingine na mwishoni mwa mwaka naweza kutoa wimbo mwingine.” Roma amefafanua.
Akieleza sababu za kubadili mfumo wa utoaji nyimbo na kutoa nyimbo tatu ameeleza kuwa amembidi afanye hivyo kwa kuwa alikuwa anaamua kuwa kimya kwa matakwa yake lakini watu wanahitaji ladha zaidi kutoka kwake kwa mwaka, na pia anataka kuonesha kuwa naye anaweza kutoa nyimbo zaidi ya moja kwa mwaka kama wanavyofanya wasanii wengine Tanzania.
No comments:
Post a Comment