Wakati nafasi yake katika jamii ikizidi kushamiri kila kukicha, msanii nyota na malkia wa filamu nchini Tanzania Salma Jabu Nisha maarufu “NISHA”, amejikuta katika wakati mgumu tena baada ya baadhi ya mashabiki wake kumlalamikia kuwa imefika wakati hata anashindwa kuwanao karibu kama
ilivyokuwa awali kabla ya jina lake kuwa katika chati.
Katika kuhakikisha
yakuwa jambo hili linapata ufafanuzi wa kina, msombe blog imepata nafasi ya
kumtafuta star huyo na hivi ndivyo mambo yalivyokwenda:
MHARIRI: Huhari gani
malkia wa bongo?
NISHA:
Hahahaaa!!! Poa sana ndugu yangu, mwenyezi anatupa uzima.
MHARIRI: Vyema
sana, kwanza tuzungumzie kidogo filamu yako ya GUMZO, ipo sokoni kwa sasa, vipi
mapokeo ya mashabiki?
NISHA: Inshaallah
Mungu anatenda mambo yake, najua hata siamini namna ambavyo mapokeo yamekuwa
makubwa..! yaani nafuraha isiyo kifani, watu wanapiga picha kisha wananipostia
katika kurasa zangu za mitandao ya kijamii, basi ni firaha tele.
MHARIRI:
Unafikiri kuwa filamu hii itasababisha kukuza zaidi sanaa ya bongo ikiwa ni
pamoja na kukujengea zaidi heshima katika kazi zako?
NISHA: Mmmh!!
Nawezasema ndiyo, kwasababu hadi sasa naona jinsi navyozidi kupata mashabiki
wengi katika kona mbalimbali za dunia,
hivyo basi inanipa shauku ya kuzidisha juhudi katika kazi zangu zote ili
nisiwakwaze mashabiki wangu.
MHARIRI: Naam!
Kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa baadhi ya mashabiki zako wakisema unajitenga
sana mbali nao tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo mlikuwa mkishirikiana
kwa mambo tofauti tofauti, hii iko vipi??
NISHA: Hahahaaa!!
Acha mambo hayo bwana, mbona mimi sipo hivyo, kwanini unasema hivyo?
MHARIRI: Kwahiyo
hizi stori ni zauongo?
NISHA:Hapana,
lakini ukweli nikuwa kuna mambo mengi yanakuwa mtu yanakukabili kwa wakati
Fulani hivyo basi unalazimika kutumia muda mwingi sana katika kuyakamilisha, na
sikuwa nafanya kuwatenga ama kuwa mbali nao. Jambo lingine ni kwamba nawapenda
sana mashabiki wangu kwahiyo wajue yakuwa napambana sana kwaajili yao ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha wanapata radha nzuri kupitia kazi zangu.
MHARIRI: Mambo
gani hayo yanakupa ubize zaidi wakati muda kama huu umeshatoa filamu basi ni
kukaa kusubiri mapato?
NISHA: Unajua siyokwamba
nakaa kutegemea filamu pekee, nina biashara zangu tofauti kabisa na sanaa,
hivyo basi wakati kama huu ndiyo huwa natumia katika kuhakikisha kila kitu
kinakwenda vyema.
MHARIRI: Biashara
gani hizo unazojihusisha nazo?
NISHA: Aaah!!
Bwana..! Ok, nafanya biashara tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na saluni yangu
iliyopo sinza ambapo ni maalum kwa maswala ya urembo.
MHARIRI: Kuna
moja ya andiko lako katika mitandao ya kijamii uliwahi kusema utawapeleka
mashabiki wako Zanzibari, embu ifafanue kwa kina imefikia wapi?
NISHA: Naaam!! Ni
kweli kabisa ndugu mwandishi, kama nilivyokujuza hapa awali yakuwa nawapenda
sana ten asana mashabiki wangu, hivyo basi katika kuhakikisha natoa walau
shukrani kidogo kwao mimi pamoja na uongozi wa kampuni yangu ya NISHA’S PRODUCTION tukaona ni vyema
kama tukifanya jambo hilo ikiwa ni sehemu ndogo tu ya kusema asante.
MHARIRI: Walengwa
haswa wa zawadi hii ni wakina nani?
NISHA: Kila
mtanzania na asiyekuwa mtanzania ilimladi anamapenzi na Nisha anakaribishwa
kujiunga nami ili aweze kupata nafasi hii. Kikubwa ni yeye kujiunga katika
kurasa zangu za mitandao ya kijamii kisha anaweza kuipata nafasi hiyo na
mwishowe NISHA’S PRODUCTION
itahakikisha anamtimizia kila kitu.
MHARIRI: Kuna
idadi ya washiriki katika safari hiyo?
NISHA: Hapana,
mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na Team Nisha na wale wote watakao patikana
basi safari ya Zanzibar itakuwa inawahusu pia.
MHARIRI: Una
maneno yapi kwa mashabiki wako?
NISHA: Nasema
tuzidishe upendo kwa wote na watambue yakuwa nawapenda sana kuliko
wanavyofikiri wao, pale napokuwa nikiwakosea waniambie ili tuzidi kuboresha
uhusiano bora kila kukicha, Napia wasisahau kwa wale ambao hawajajipatia nakala
ya GUMZO basi wafanye hiyana
kuipata. Mmwaaa!!!!!!
No comments:
Post a Comment